Habari

Picha: Ni kweli Nicki Minaj amechumbiwa na Meek Mill?

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni je ni kweli Onika Tanya Maraj a.k.a Nicki Minaj amevishwa pete ya uchumba na Meek Mill?

Nicki n meek

Baada ya Minaj kupost picha ya mkono wake wa kushoto Instagram inayoonesha pete ya almasi yenye umbo la moyo kwenye kidole chake cha chanda, hisia zimeibuka kuwa ile ni pete ya uchumba inayoaminika amevishwa na anayedaiwa kuwa boyfriend wake Meek Mill.

Nicki Minaj ring
Picha aliyopost Nicki Minaj

Nicki na Meek wote hakuna aliyethibitisha moja kwa moja kama sasa ni wachumba, lakini kwenye picha hiyo hakuandika chochote zaidi ya kuweka emoji za moyo na pete.

Wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja wakila bata, wakisafiri na kufanya show na kushare picha za wawili kila mara.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents