Bongo Movie

Haiwezekani kufahamika kimataifa bila management – Irene Paul

Msanii wa filamu, Irene Paul amesema sio kazi rahisi kwenda kimataifa bila kuwa na management.

11117151_1581004155490417_1672267217_n

Amesema umefika wakati wa kutafuta management ya itakayosimamia kazi zake pamoja na kuhakikisha anapiga hatua kimataifa zaidi.

Akizungumza na Bongo5, Irene alisema amejipanga kutafuta timu ya kuongoza kazi zake na kumtafutia masoko mapya.

“Mimi sasa hivi nipo kwenye mchakato wa kutafuta management itakayonisaidia kufika mbali zaidi hasa hasa kimataifa. Kama unavyojua sio rahisi kufika huko mwenyewe na ninakubali mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao siwezi kufika huko binafsi,” alisema.

“Unajua mimi ni msanii, mimi sio manager, sio marketing person, inabidi ifikie wakati kila mtu ashukuru karama aliyopewa na Mungu wake. Mimi karama yangu kubwa ni weka kamera nikuonyeshe kazi, lakini napenda kufika mbali na siko vizuri kwenye marketing nipo kwenye process ya kutafuta watu wa kufanya kazi na mimi, kuanzia marketing, manager pamoja brand person ambaye atani-brand mimi pamoja na baadhi ya kampuni zangu. Kwahiyo nahitaji full package ya team ambayo itanisogeza mbele zaidi,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents