Picha: Osse Greca Sinare vs Gavin Gosbert – Nani mpiga picha bora zaidi Tanzania?
Ukimtoa Raqey wa I-View Studios, huwezi kuacha kuwataja Gavin Gosbert na Osse Greca Sinare kama wapiga picha bora zaidi nchini Tanzania. Vijana hawa ambao wote wapo chini ya miaka 30 wamejichukulia umaarufu kwa ustadi wao wa kupiga picha maridadi na kuzitengeneza kuzipa mvuto katika muonekano wake wa mwisho.
Wote wana makampuni yao yanayofanya kazi za upigaji picha za mitindo, matangazo ya biashara na matukio mbalimbali. Lakini kati ya Osse na Gavin, ni nani mpiga picha bora zaidi? Tazama picha zao na kisha umtaje mwenye picha za kuvutia zaidi.
Osse Greca Sinare
Osse
Osse Greca Sinare ni mpiga picha wa fashion aliyeshinda tuzo ya ‘Fashion Photographer of the Year 2012’ ya Swahili Fashion Week. Pia jarida la Teenspot lilimtaja kwenye orodha ya ‘10 Most Powerful Youth in Tanzania for 2012.’
Osse ni mwanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya OGS Multimedia studio inayojihusisha na upigaji picha na utengenezaji wa graphics. Kupitia kampuni yake, Osse ameshafanya kazi na makampuni kama Akemi | Tanzania’s Revolving Restaurant, Precision Air In-flight Magazine, Vodacom, Hassan Maajar Trust, Bang Magazine, Bank M, Maznat Bridal Salon na pia akiwa kama mpiga picha wa Teenspot Magazine.
“My work is inspired by many things I experience and see from day to day activities. I could see an abandoned apartment or children playing in the playground and it would instantly trigger an idea for me to try out. I always spend countless hours on-line searching for inspiration from other artist and magazines for constant inspirations,” ameandika kwenye profile yake.
“The type of photography that inspires me is high end fashion, and vintage, dreamy almost surreal. I love all the different beauty you can find in people and love sharing that with others in my photos.
I pride my work not on the technical ability but more on my creativity and the valuable people that contribute to my ideas. I love the whole process of the idea creation to the finish of a project, it truly excites me. Photography is my passion and always will be.”
Baadhi ya picha alizopiga:
Gavin Gosbert aka Soul Kid
Gavin
Gavin aka Soul Kid anatokea Arusha na alizaliwa miaka 26 iliyopita.Ni mpiga picha aliyejifunza kwa utundu wake mwenyewe. Ni msanii wa graphics na pia ni cinematographer. Alitajwa kuwania tuzo za Under 30 Youth mwaka 2013 kwenye kipengele cha designing.
“I am thankful to God for gracing me with the opportunity to establish my very own company with my colleague Melchizedech, registered as Black n White Visual Studios. Throughout the year I’ve had the chance to work with many clients like, Teenspot magazine, Paa magazine, Dar Life magazine and Clouds Media company,” ameandika kwenye profile yake.
I’m honored to have met wonderful people like Andrew Mahiga, Amin `Swai, Vanessa Mdee, Jokate Mwigelo, Maria Sarungi, Lisa Jensen and a lot more who have inspired me in many ways in all walks of life.”
Baadhi ya picha alizopiga: