Burudani

Picha: Shetta aenda Afrika Kusini kushoot video ya collabo yake na Kcee wa Nigeria

Mwaka jana (2014) Shetta aliahidi kuwa single yake itakayofata itakuwa ni collabo na rapper wa Nigeria, ahadi ambayo inaonekana tayari imetimia.

Kcee & Shetta
Kcee na Shetta

Kwa mujibu wa picha alizoshare rapper Kcee wa Nigeria akiwa na Shetta nchini Afrika Kusini, inathibitisha kuwa collabo hiyo iliyopewa jina la ‘Shikorobo’ sasa iko katika hatua za uchukuaji wa video.

Kupitia Instagram hit maker wa ‘Limpopo’ Kcee alishare picha aliyopiga na Shetta na kuandika”

“Work mode: on set with my bro @shettatz no time”.

Shetta & Kcee
kcee

Na kwenye picha yao nyingine Kcee aliandika:

“Chillin with my nigga #baddest boy from Tanzania @shettatz #Jozlife….., #GOODBOYFRIEND”

Katika mahojiano na Global TV, September 2014 Shetta alisema kuwa (kwa wakati huo) wimbo huo ulikuwa tayari na alichokuwa anakisubiri ni Kcee kuingiza sauti yake.

“Nizungumze kwamba kuna project mpya inakuja[…] kuna collaboration kubwa nitaifanya na Mnigeria mmoja surprise sasa hivi siwezi kumtaja.”

Shetta aliongeza kuwa mtu aliyemsaidia kumuunganisha na Kcee ni Diamond Platnumz (Ingia hapa).

Bado haijajulikana video hii mpya ya Shetta na Kcee inafanywa na director gani, lakini video iliyopita ya Shetta ft. Diamond ‘Kerewa’ iliongozwa na Godfather na kufanywa huko huko Afrika Kusini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents