Burudani

Picha: Times FM, Naibu Waziri wa Ajira na wanachuo wajumuika kuzijadili changamoto za ajira

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde Jumamosi hii amekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kujadili changamoto za ajira nchini lililoandaliwa na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM na kuwahusisha wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu mbalimbali nchini.

IMG_7684

Kongamano hilo pia liliendana na uzinduzi wa kipindi hicho kinachoruka kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu usiku na kuongozwa na Raheem Da Prince na Sandra Temu.

IMG_7709
Watangazaji wa kipindi cha Campus Vibes, Sandra Temu na Raheem Da Prince wakiongoza mjadala maalumu wa utakaoibua hoja ya kutatua changamoto ya ajira nchini

Akiongea kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, mheshimiwa Mavunde pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu wa muda. “Muda ni kitu cha msingi na kukitunza sana,” alisema.

IMG_7688

“Nilikuwa na ndoto ya kuja kuitumikia jamii, nilikataa kazi nyingi za kuajiriwa ili kuifuata ndoto yangu, nilikuwa naamini maisha yangu yapo kwenye siasa, mpaka sasa niliitambua njia yangu na ndio njia niliyopitia,” alisisitiza.

13649200_620849661414194_673435438_n
Mhe. Mavunde

Kwa upande wake MC Pilipili ambaye pia alikuwa mmoja wa wazungumzaji, alisema kuzaliwa kwenye familia maskini hakumaanishi kuwa huwezi kujinasua na kuwa na maisha unayotaka.

IMG_7700
Mc Pilipili akijitambulisha kwa vijana, pembeni yake ni Ron Fidanza na Mhe. Anthony Mavunde

“Usikasirike kuzaliwa katika familia ya kimasikini sio kosa lako, jukumu lako ni kujiondoa katika umasikini,” alisema mchekeshaji huyo ambaye pia ni mtangazaji wa kituo hicho cha redio.

IMG_7679
BAADHI ya wanafunzi wa elimu ya juu kutoka katika vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam waliohudhuria kongamano hilo

“Mungu kila mtu kampa kipaji angalia jambo gani linajitokeza sana katika maisha yako, usifate mkumbo, niliamua kukifata kipaji changu katika kuchekesha.”

Naye Meneja wa vipindi Times Fm, Ron Fidanza aliezea mchango wa kipindi cha Campus Vibes kwa wanafunzi wa chuo: Times Fm imejikita kutoa mchango wake kupitia kipindi cha Campus Vibes ili kujenga jukwaa la mazungumzo kwa vijana na wanafunzi wa elimu ya juu,” alisema.

IMG_7702
Msimamizi mkuu wa Times FM, Ron Fidanza

“Pia Times Fm imeanzisha program maalum ili kuwawezesha wasomi wa habari vyuo vikuu kufanya mazoezi kwa vitendo.”

Picha ma Cathbert Kajuna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents