Habari

Picha: Vilio na simanzi vya tawala kuaga miili ya wanafunzi 32 Arusha

Ni vilio na simanzi zimetawala katika kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu 2 pamoja na dereva mmoja waliopoteza maisha kwa ajili ya gari Jumamosi hii huko mkoani Arusha.

Wananchi wakiwa amejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sheikh Abeid Karume Arusha kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko mjini Arusha muda huu ambapo anaongoza wananchi wa mkoa huo pamoja na mikoa ya jirani katika kuuaga miili ya wanafunzi 32, walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Vincent iliyopo mkoani humo.

Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Miili ikishushwa ndani ya gari
Mama akisaidiwa na watu wa msalaba mwekundu baada ya kuanguka
Ni simanzi na vilio
Baadhi ya wazazi wakisadiwa
Baadhi ya viongozi wakiwa katika msiba huo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents