Michezo

Picha: Wawili waondoka na Bajaj TVS King kutoka SportPesa

Mkazi wa Kijichi jijini Dar es salaam, Hassan Musa Vidallah pamoja na Haidary Mrisho mkazi wa Tanga wameibuka na kuondoka na  Bajaj TVS King kutoka SportPesa.

Kushoto ni SportPesa Casper akifatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Mr Tarimba Abbas, Mke wa Hassan, Salma Bakari (23yrs) pamoja na mshindi wa TVS KING BAJAJI Hassan Mussa Vidallah (24yrs).

Wawili hao kila mmoja alikabidhiwa bajaj yake na uongozi wa SportPesa baada ya kutangazwa kuwa washindi.

SportPesa kupitia promotion yake ya ShindaNaSportPesa inatoa bajaj moja kila siku kwa wateja wake ambao wanatumia huduma za kampuni hiyo.

Akizungumza na mtandao huu, Hassan Mussa Vidallah amesema bajaj hiyo itabadili mfumo wa maisha ya familia yake kwa ujumla.

“Mimi na mke wangu tunawashukuru sana SportPesa kwani wanaenda kubadili maisha yetu, Siku ya kwanza kuona ilikuwa mshindi kutoka tanga aitwaye Cassian Anthony ambaye aliweka kwenye mtandao wake wa kijamii Instagram akisema ameshinda bajaji, ilibidi nimfate pembeni kwenye message ya kawaida na kumuuliza ni jinsi gani alicheza na kushinda, Cassian hakuwa mchoyo kwani alinielekeza na nikaingia kwenye ukurasa wa SportPesa ili kupata taarifa zaidi jinsi ya kushiriki promosheni hii.” alisema Vidallah.

Aliongeza, “Kikubwa ni imani nilikuwa na imani kwamba kama ninavyoona watu wakitoa ushuhuda kwamba wanashinda basi na mimi ipo siku nitashuhudia ushindi wangu kwa watu na kweli imetokea. Siwezi kuiongelea furaha yangu maana hii bajaji itanisaidia kufanikisha mambo yangu mengi sana ikiwemo kuisaidia familia yangu pamoja na wadogo zangu kuwaendeleza na masomo kwani sisi kwetu wengi tumeishia kidato cha nne hivyo hii itakuwa moja kati ya njia itakayo niingizia kipato ukiacha na kazi yangu ya sasa hivi ya kuuza dawa za tiba mbadala.”

Mtangazaji wa kipindi cha SportPesa Happiness Wandellah kinachorushwa kila siku Clouds TV usiku na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa Tanzania Adventina John wakimkabidhi mshindi kutoka Tanga wa TVS KING DELUXE     Ndugu Haidary Mrisho(39)

Kwa upande wa mshindi mwingine, Haidary Mrisho ambaye ni mfanyabishara mdodo mdogo, bajaj hiyo itaweza kumsaidia katika biashara zake.

“Mimi natumia sana laptop na simu hivyo nilijifunza jinsi ya kujiunga ingawa mwanzoni nilikwama nikawapigia huduma kwa wateja SportPesa na wakanipa ushirikiano mzuri sana kwakweli.” alisema Haidary Mrisho.

Aliongeza, “Nilikuwa siamini kabisa kama nimeshinda ukweli ingawa namba yangu ilionekana kwenye tv na sikuhiyo nilipigiwa simu na watu wengi sana hata wengine ambao siwafahau kutoka mikoa tofauti mfano Mtwara, Mpanda, Tanga na nikawaeleza ni kweli yani hata mimi siamini, mpaka hii leo mlivyoniambia mko njiani mnakuja sikuamini hadi sasa hivi mlivyofika na bajaji yangu”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents