Michezo

Pitso Mosimane atunukiwa Udaktari wa Heshima

Chuo kikuu cha Johannesburg, Afrika Kusini kimemtunuku Udaktari wa heshima aliyekuwa Kocha wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly Pitso Mosimane kutokana na mchango wake mkubwa kwa jamii kupitia mchezo wa mpira wa miguu.

Hayo yamethibitishwa na Taasisi ya MT Sport Marketing and Management ambayo inamsimamia Kocha huyo ambaye ametwaa mataji makubwa ya kitaifa na Kimataifa akiwa na vilabu hivyo  kabla ya kutimkia mashariki ya kati.

Akiwa mchezaji Pitso amecheza Vilabu vya Jomo Cosmos, Mamelodi Sundowns, Orlando Pirates, Ionikos, KFC Rita na Al Sadd pamoja na Timu ya Taifa ya Afrika Kusini akiwa amecheza jumla ya mechi 183 na kufunga mabao 52.

Akiwa kocha Pitso amefundisha vilabu kama Supersport United, timu ya taifa Afrika Kusini (Msaidizi), Mamelodi Sundowns, Al Ahly, Al Wahda, Abha Club hadi sasa.

Pia akifundisha amefanikiwa kushinda mataji kama ligi ya Mabingwa Afrika mara 3, CAF Super Cup mara 3, ligi kuu Afrika Kusini mara 5, Saudi FDL na kuipandisha timu daraja, Egypt Cup, Nedbank Cup mara 3, Telcom Cup bila kusahau tuzo binafsi za ndani na za kimataifa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents