Burudani

Professor J anaamini wadogo zake wanaweza kuwa wanasiasa wazuri pia

Rapper na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule aka Professor J amesema wadogo zake wakiamua kuingia kwenye siasa wanaweza kuchukua nyadhifa za juu hata urais kutokana na uwezo wao.

Professor akiwa kwenye shughuli za kisiasa

Professor ambaye ni kaka wa Black Rhino, Simple X na wengine, amekiambia kipindi cha XXL kinachoruka kupitia Clouds FM kuwa, wadogo zake wana uwezo mkubwa wa kufanya vitu vikubwa hata zaidi yake.

“Ujue uzuri ni kwamba baba yetu alitupa urithi mmoja mkubwa sana ambao ni urithi wa elimu,” alisema J.

“Kwahiyo hata sisi tupo hivyo na mara nYingi ukimsikiliza Black Rhino, ukimsikiliza Simple X, ukimsikiliza Kiliombio wote unawaona ni vijana ambao wamepevuka na ni watu ambao wanatumia akili maana yake wameenda shule na wamepata elimu ya kutosha.”

Aliongeza, “Kwahiyo kufanya siasa ni maamuzi ya mtu binafsi kwamba kama mtu anaweza akafanya siasa anaweza kufanya. Rhino sijui kama anataka kufanya siasa hiyo anatakiwa kuielezea mwenyewe anaionaje, lakini kiukweli wote niliwavutia kwenye muziki na wakafanya muziki vizuri kwa kiwango cha juu na mbaya zaidi walikuwa wanafanya katika kiwango ambacho hata kinanipita mimi kwa kiwango cha juu sana. “

“Sasa mimi nimeingia kama Mbunge wa Mikumi huenda wao wakaja kuwa maraisi wa Tanzania kwa sababu watakuja kufanya siasa kwa kiwango cha juu kwa sababu wana elimu ya kutosha na wana maono ya kutosha na wengine wanafanya kazi kwenye mabenki makubwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents