Burudani

Queen Darleen aelezea sababu za kupoteza fahamu kwenye show ya uzinduzi wa video yake (Audio)

Furaha, pressure, ukumbi kujaa kuliko alivyotarajia na surprise kutoka kwa kaka yake Diamond Platnumz kwenye ukumbi wa Bilicanas Jumapili iliyopita kwa pamoja vilimfanya Queen Darleen apoteze fahamu.

Queen Darleen na Diamond

Akiongea na Bongo5, Queen amesema wakati anajiandaa kupanda stejini alishangaa kumuona Diamond akipanda stejini na Shetta wakati alikuwa anafahamu kuwa kaka yake huyo yupo nchini Nigeria. Amesema sababu nyingine ni namna ukumbi ulivyokuwa umejaa kiasi ambacho hakutegemea kama ingekuwa hivyo.

“Sikutegemea kweli kama ningepata watu wengi kiasi kile, nafikiri katika mwaka huu tangu uanze hakuna aliyefunga rekodi zaidi yangu mimi halafu ukizingatia mimi ni mwanamke ujue,” amesema. “Sasa kila mtu akawa anakuja ‘hatari, kuna watu wengi sana, watu wanazidi na nafasi hakuna’ kwahiyo maneno ya watu yakawa yananichanganya, unajua kuna mtu mwingine anakuja ‘fanya show ya uhakika’. Baada ya kumuona Nasib pale ndio nikawa nimepata shock. Yeye ndio akaniambia ‘sikiliza nikuambi dada yangu, usiogope usifanye nini, fanya show nzuri.”

Anasema kitendo cha kumuona kaka yake huyo kilimfanya alie machozi ya furaha kwakuwa hakutegemea kama angekuwepo kumpa support.

Ameongeza kuwa show hiyo imemfanya agundue kuwa kumbe ana mashabiki wengi na hivyo anatakiwa kuuchukulia muziki serious zaidi kuliko alivyokuwa akifanya mwanzo na kwamba tangu afanye show hiyo amepata simu nyingi kutoka kwa mapromota wengine akafanye show akiwemo promota kutoka DR Congo.

Msikilize zaidi akiongea hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents