Habari

Rais Magufuli aagiza nchi yoyote itakayozuia maziwa ya Tanzania nayo izuiwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuwa nchi yoyote itakayozuia maziwa ya Tanzania nayo izuiwe kuingiza maziwa yake hapa nchini.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi kabla ya kufungua kiwanda cha kuzalisha saruji cha Kilimanjaro kilichopo katika eneo la Maweni Mjini Tanga.

Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage kuchukua hatua dhidi ya kiwanda cha maziwa cha Arusha ambacho baada ya kubinafsishwa kimegeuzwa kuwa kituo cha kukusanyia maziwa na kuyasafirisha nje ya nchi kwa ajili ya kusindikwa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents