Habari

Rais Magufuli aijibu kampeni ya kuziba midomo ya wabunge wa upinzani (Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameijibu kampeni iliyoanzishwa na upinzani ya kuziba midomo yao kudai kuwa serikali ya awamu ya tano imekosa demokrasia.

Alikuwa akihutubia Alhamis hii ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita.

“Niwaombe wanasiasa wenzangu, ushindani wa sasa hivi wa vyama vya siasa ambao unatakiwa upigiwe nguvu zaidi ni kwa wale wawakilishi waliopewa mamlaka na wananchi. Kama ni kwa madiwani wakapeleke hoja kwa nguvu sana kwenye maeneo yao,” alisema.

“Kama ni wabunge wakazungumze kwa nguvu zote bungeni lakini hata kuziba midomo nayo ni demokrasia,” aliongeza na kusababisha kicheko kwenye ukumbi wa ikulu jijini Dar.

“Kwahiyo hiyo ndio demokrasia ya muelekeo ya aina yake.”

2

Hivi karibuni, wabunge wa upinzani walisusia vikao vya bunge na kuziba midomo yao kwa makaratasi wakidai kutokuwepo kwa demokrasia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents