Habari

Rais Magufuli ametoa nafasi za ajira zaidi ya 50,000 – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mheshimiwa Rais Magufuli ametoa nafasi za ajira zaidi ya 50 elfu ili kuziba mapengo yaliyojitokeza kwenye vyeti feki.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu maarufu kama maswali ya Papo kwa Papo.

“Muheshimiwa Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli, ametoa nafasi za ajira zaidi ya 50 elfu ili kuziba mapengo ambayo yamejitokeza kwenye vyeti feki lakini kuongeza tu ajira kwenye sekta nyingine kwa maana kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwenye sekta mbalimbali na tayari vibali vimeshatolewa katika wizara ya Utumishi tumeanza na idara ya elimu,” alisema Majaliwa.

“Tumeshaajili walimu wa masomo ya Sayansi wamekwenda kwenye vituo tumetoa pia nafasi kwenye sekta ya afya na vibali hivi vitaendelea kutolewa kadri ya nafasi ambazo Muheshimiwa Rais ameahidi kwa Watanzania, na naamini Rais wetu mpendwa kwa ahadi yake nafasi hizi ataendelea kuzitoa kuziba mapengo na kuboresha pale ambapo kuna upungufu mkubwa na sasa ajira hizi zitaenda kitaaluma zaidi ilikuweza kuleta ufanisi mkubwa kwenye sekta ya ajira.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents