Habari

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jumatano hii  alimteua Doto M. James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

1

Kabla ya uteuzi huo James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

 Doto M. James ameapishwa leo  Septemba 1, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents