Burudani

Rais Obama abandika picha aliyopiga na Sauti Sol wakicheza ‘Sura Yako’ kwenye ukuta wa White House

Mafanikio kwa bendi ya Sauti Sol ya Kenya yanazidi kuonekana siku hadi siku.

Sauti-Sol-Obama-2

Kwa mujibu wa Sauti Sol, Rais Obama amebandika picha aliyopiga na bendi hiyo wakicheza hit song yao ‘Sura Yako’, kwenye ukuta wa White House ya Marekani. Picha hiyo ilipigwa wakati wa ziara ya Obama nchini Kenya miezi miwili iliyopita ambapo Sauti Sol walipata nafasi ya kipekee ya kutumbuiza.

Sauti Sol wameshare na ulimwengu habari hiyo kupitia Twitter.

“Dreams come true. A picture of us dancing with President Barack Obama has been placed in the The White House You will see it when you take a tour of the West Wing, right near the Oval Office!”

sautisol tweet

Bendi hiyo kwasasa wameachia ngoma mpya ‘Isabella’, ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki wao sehemu mbalimbali za Afrika na nje.

Enjoy wimbo wao mpya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents