Habari

Rais Samia atoa sababu ya kuwaacha Lukuvi na Kabudi kwenye listi ya mawaziri

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza sababu za kuwaacha katika listi ya mawaziri kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na. Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri Palamagamba Kabudi.

”Nina kaka zangu wawili, William Lukuvi na Kabudi ukiwatazama hawa umri wao kama wangu na mkitizama niliyowateua hamfanani kabisa kwa hiyo kaka zangu wawili hawa nimewavuta waje kwangu ili waje wanisimamie kuwasimamia ninyi.”

”Kwa hiyo kuwaacha kwangu kwenye hiyo listi ni kwasababu hapa wote wadogo wadogo na mnahitaji kusimamiwa vizuri kwa wawili wale watakuja kwangu kuwasimamia ninyi vizuri, lakini jingine kaka yangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia mazungumzo ya Serikali na Mashirika na ndiyo kazi ambayo sasa ninataka nimkabidhi kindakindaki aendelee na kazi hiyo, ila kwa sababu kazi yake haipo kwenye muundo haitangazwi wala nini lakini atasimamia hiyo kazi.”

”Mashirika yote kazi zote zitakazo ingia ubia na Serikali kabudi ataongoza hiyo timu, kwa hiyo yeye ni baba mikataba, baba maelewano. Kaka yangu Lukuvi yeye ana kazi na mimi mtaisikia baadae, lakini namvuta Ikulu kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.”

”Kwa sababu nikiwatazama hapo wote wanakaribia kustaafu wengine bado miaka miwili, wengine mnasafari ndefu mimi na wale tushastaafu kazi yetu ni kushika kiboko kuwasimamia nyie na Makatibu wakuu.”

”Msikae hapo mnasema, nimeona meseji nyingi afadhali Lukuvi katoka, hajatoka yupo wengine wameanza kumletea meseji za ajabu ajabu wakijua atagombania Spika, hatagombania anakazi na mimi, kwahiyo hatakuwa Spika wala hatagombania msianze kumchafua, ametumikia taifa hili kwa uadilifu kwa muda mmrefu mmuache aende na mimi tumalize kazi atakayopangiwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents