Habari

Rais wa zamani wa Korea Kusini atishiwa kifo

Serikali ya Korea Kaskazini imemtishia kifo rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun Hye na mpelelezi wake na kuwaambia kuwa wanaweza kufa vibaya saa yoyote.

Pyongyang ilitoa onyo hilo siku ya Jumatano baada ya kumshutumu Bi Park na Mkurugenzi wa NIS Lee Byung ho kuhusika na njama ya kumuua kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na kutaka wachukuliwe hatua za kisheria.

Korea Kaskazini ilishutumiwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa Kim Jong Un,Kim Jong Nam kwa kutumia sumu aina ya VX katika uwanja wa ndege wa Malaysia mwezi Februari.

Korea Kaskazini imesema kuwa Bi Park anapashwa achukuliwe hatua ya kisheria na apewe adhabu yake.

Kwa mujibu wa habari,Korea Kaskazini inaamini Korea Kusini ikishirikiana na Marekani zilikuwa zina mpango wa kummaliza kiongozi wa Korea Kaskazini ambae hulindwa kwa hali ya juu katika nchi yake.

.Korea Kaskazini imesema kuwa japokuwa Marekani na Korea Kusini zinadharau onyo hilo hivi karibuni nchi hizo mbili zitaipata adhabu yake.

Hata hivyo Korea Kusini imesema kuwa vitisho vya Korea Kaskazini havina maana na haitoruhusu madhara yoyote kuwapata raia wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents