Habari

Ray C is Back: Atuma ujumbe muhimu kwako, aonesha alivyobadilika, unaweza kumsahau (picha)

Mwanamuziki staa wa bongo fleva Rehema Chalamila a.k.a Ray C amepotea katika anga ya muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya na baada ya kupata tiba sasa mambo yanaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida.

Ray C-batural hair

Pamoja na ukimya wake katika muziki, Ray C a.k.a kiuno bila mfupa sasa anaonekana kuwa active zaidi katika mitandao ya kijamii hususan Instagram. Ray C ameshare baadhi ya picha na fans wake kupitia instagram ambazo kwa namna moja au nyingine zinaongea zenyewe (kwa kusindikizwa na captions) juu ya maisha yake ya sasa. Kwa ufupi ni kuwa Rehema anakula bata tu sasa hivi, thanks kwa shavu alilopewa na Rais Jakaya Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’. Take a look….

Hizi ni baadhi ya picha zinazomwonesha yeye mwenyewe alivyo sasa, amenenepa sana!

Ray C-no caption

Ray C - Me my self n I
“rayc1982 Me myself n I”

Ray C - Me my self n I 2

Ray C- no caption 3

Ray C - I love my hair......
“rayc1982 I love my hair……”

Ray C - I have fat legs
“rayc1982 I have fat legs”

Ray C-no caption2

Ray C - I did it
“rayc1982 I did it yeah#goofingaroundwithmyipod#playingaround#funtimes”

Mwili haujengwi kwa mawe wala matofali, kwa afya uliyomwona nayo Ray C sio jambo la kushangaza kama hii ndio menu yake ya kila siku. Hizi ni baadhi ya picha za vyakula ambazo amepost katika akaunti yake:

Ray C -  My late lunch# pilauchicken#instafood
“rayc1982 My late lunch# pilauchicken#instafood”

Ray c viazi vitamu na nazi
“rayc1982 Viazi vitamu na nazi!”

Ray C - yummy
“rayc1982 Yummy#chocolateaddict#chocolatecake#chocolatefan”

Na huu ndio ujumbe ambao Ray C ameutuma kwa mashabiki wake wote waliomsapoti katika muziki wake kipindi chote:

Ray C - msg

Ray C pia aliweka picha ya first lady wa Ruff Ryders E.V.E na boyfriend wake wa kizungu na hapa ndio alifunguka juu ya mapenzi aliyonayo kwa wanaume wa kihindi na wazungu na kusema hapendi wanaume wa kiswazi.

ray insta
“My girl Eve..Ruff Ryder’s First Lady E.v.E with her British Boyfriend Max!She Loves White Boys Uwiii Same here!”

Baada ya kuweka picha hiyo na caption mtu mmoja akamuuliza, “@rayc1982 I thought you loved Indians?”

Hapo ndio akafunguka, “ Wote atakaejitokeza huyohuyo Kati ya muhindi na Muzungu bt mswaz no @imbayalinda”.

Haya kazi kwako kama wewe ni “mswazi” na ulikuwa una ndoto siku moja macho ya kimahaba ya Ray C yaje kukudondokea pole sana sababu bibie ameshatoa vigezo vyake.

Pia Ray C aliweka picha ya Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Marekani Barack Obama alipoitembelea Tanzania wiki hii, na akaandika caption hii “rayc1982 My daddy with the one n only Obama!am proud!”

Ray C-my daddy n Obama

Mwezi (December) 2012 Ray C akisindikizwa na mama yake Magreth Mtweve alimtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam kwa lengo la kumshukuru kwa msaada wa matibabu aliompatia baada ya kupata matatizo yaliyotokana na matumizi ya madawa ya kulevya kama ilivyoripotiwa na vyombo vingi vya habari.

Na hii ndiyo picha waliyopiga na Rais Ikulu (December) mwaka jana.

Ray C Ikulu

Picha zote Ray C kaziweka katika akaunti yake ya Instagram kati ya wiki mbili zilizopita na leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents