Burudani

Raymond: Kufanana kwa maneno na wimbo ya Harmonize ni kawaida

Label ya Wasafi imeanza kufanya vizuri baada ya kumtambulisha vizuri Harmonize, lakini sasa wamemtambulisha msanii mwingine anayejulikana Raymond.

raymond_kwetu_Download

‘Kwetu’ ya Raymond, ni moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri kwenye media mbalimbali. Kuna baadhi ya maneno kwenye wimbo huo kama ‘Bado’ limetajwa sana huku neno kama hilo likiwa ni jina la wimbo wa Harmonize aliomshirikisha Diamond Platnumz.

Akizungumza na Bongo Kali, inayoruka kupitia City FM Radio, Raymond amesema, ‘hilo ni neno ambalo lipo sijalitoa kwenye wimbo wa Harmonize.’

“Wakati Harmonize anarekodi wimbo wake mimi sikuwepo, lakini hata wakati narekodi wimbo wangu Harmonize hakuwepo pia kwa sababu kuna session tofauti studio. Hilo ni neno ambalo lipo tu kwani hata Chege aliwahi kuimba ‘Mambo Bado’,” ameongezea.

“Video ya wimbo wangu ‘Kwetu’ ipo tayari, tumefanya nchini Afrika Kusini na director Godfather,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents