Burudani

Snura adai hataki tena kuzaa nje ya ndoa

Msanii wa muziki, Snura Mushi amesema kuwa hataki apate mtoto mwingine hadi atakapoolewa.

SNURAAAA

Muimbaji huyo ambaye ni mama wa watoto wawili, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa kwa sasa anataka mwanaume mwenye maadili na imani.

“Mimi ni mwanamke, nina watoto wawili kwa sasa na ninatamba na wimbo wangu mpya wa ‘Chura’, lazima nitamani kuolewa lakini sitamani kuwa na mtoto mwingine nje ya ndoa, nataka niolewe na mwanaume mwenyewe awe na imani, mapenzi kwangu na kazi yangu kwa ujumla,” aliesema Snura.

Snura alisema anaamini mwanaume akiwa na imani atapenda muziki wake ambayo ndiyo kazi yake, atampenda yeye na familia yake lakini akikosa imani pia hatokuwa na imani naye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents