Habari

RC Makonda atoa jenereta, mabati na mipira kusaidia mpira wa kikapu Dar (+Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa, Paul Makonda leo jumanne ametoa msaada wa Jenerata ya kisasa, Mabati 150 na Mipira 110 kwa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam ili kujengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.

RC Makonda akikabithi Jenereta kwa  Mwenyekiti wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam,Okare Emesu.

Jenereta hiyo ya kisasa ina uwezo wa KV 35 na haitoi muungurumo wa sauti ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.

Nataka mkoa wa Dar es salaam uwe unaogoza maana hili ni jiji wachezaji waweze kuwa mifano pia niliahidi kuwapatia mabati pamoja na jenereta kwa ajili ya kutumika pindi umeme utakapokatika hivyo nimewapatia mabati 150 jenereta lenye KV 35 lenye uwezo wa kufanya kazi masaa 8, pamoja mipira 110,ikiwa na lengo la kufanikisha mchezo huu na kuweza kusonga mbele,“amesema RC Makonda.

Hata hivyo, RC Makonda amesema anataka kuona Timu ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa itakayotoa Wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ndani na nje ya nchi.

Uamuzi wa RC Makonda kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa Kikapu Uwanja wa Taifa na kujionea uchakavu wa bati unaosababisha Wachezaji kunyeshewa na mvua, ukosefu wa Jenereta kipindi umeme ukikatika na uhaba wa mipira hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.

Aidha RC Makonda ameahidi kujenga viwanja vitatu vya Mchezo wa Kikapu ambapo tayari ramani imetengenezwa na muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa Viwanja hivyo.

Ili kuendelea kuimarisha michezo Dar es salaam, RC Makonda amesema anaunda kamati maalumu ya kushughulikia michezo ya aina zote.

Tayari RC Makonda amepata mdau atakaejenga Swimming pool la kisasa Kinondoni kwaajili ya Mchezo wa Kuogelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam Okare Emesu amemshukuru RC Makonda kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents