Habari

RC Mwanza atoa siku 7

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ametoa siku saba kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Mkoa huo kuwasilisha kwenye vyombo vya dola majina ya wakusanya mapato ya Halmashauri ya Sengerema waliohusika na upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 350 ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Mhandisi Gabriel ametoa kauli hiyo kwenye kikao maalum cha kujadili utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuishia Juni 30, 2020, ambapo kwa kipindi hicho Halmashauri ya Sengerema ilipata hati yenye mashaka hali iliyomlazimu kutoa agizo la kukamatwa kwa wakusanya mapato hao,

Vile vile ametaka kitengo cha fedha cha Halmashauri hiyo, kikaguliwe ili kuona ni kwa namna gani wanatoa taarifa zao za mapato, kwa sababu hata yanayopatikana sasa ni madogo licha ya kuwa Halmashauri hiyo ina vyanzo vingi vya mapato.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga ameahidi kutoa ushirikiano katika kuwabaini waliohusika na upotevu wa fedha hizo, kwani wengi wao ni watumishi wa umma na majina yao tayari wanayo.

By- BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents