Burudani

Real Dolls kutengeza roboti aliye na akili bandia na mwenye uwezo wa kushiriki ngono

Kampuni ya Real Dolls inayojihusisha na kutengeneza maroboti imedai mwakani ina mpango wa kutengeza roboti aliye na akili bandia na mwenye uwezo wa kushiri ngono.

Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.

Akitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono,”Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya,”

Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema.

Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.

Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents