BurudaniHabari

RECAP: Rayvanny kuwatolea uvuvi Watangazaji baada ya kusema amezidisha Remix

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezichambua kauli kadhaa za Rayvanny aada ya kuwajibu wanaomsema kuwa ameshuka thamani kisa kufanya sana Remix au kutembelea upepo wa wasanii wenzake.

@el_mando_tz ameanza kwa kumpongeza Rayvanny akisema hajachukulia jambo hili Personal bali ameamua kuleta mjadala hadharani kuhusu mambo kadhaa yanayozungumzwa juu yake.

Anaongeza kuwa Rayvannny ametolea mfano ngoma kadhaa zilizofanywa na wasaniii tofauti tofauti za Remix na kufanya vizuri duniani huku zingine zikivunja na kuweka rekodi mbalimbali.

@el_mando_tz anasema Rayvanny asingetaja wasanii aliowataja na ngoma walizofanya kwani ni mifano tofauti na inayomhusu yeye.

Wenzake hasa kutoka Nigeria hawafanyi Remix ilimradi bali wanakuwa makini sana kwenye kuchagua wasanii wa kufanya nao Remix na mara nyingi wanaangalia hizo Remix wanazofanya zinawakuza vipi kwenye career zao??

Rayvanny kosa lake anafanya Remix na kila m tu kitu ambacho kinashusha thamani yake na kumfanya aonekane Cheap sana kwa wasanii wenzake.

Remix yake na Maluma ilikuwa sahihi sana na angetakiwa akazie pale pale.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents