Promotion

Rick Ross kutumbuiza MTV MAMA’s

Rapa kutoka Marekani Rick Ross aka Teflon Don pamoja na wasanii P unit kutoka Kenya wameongezwa katika orodha ya wasanii watakaotoa burudani siku ya sherehe za utoaji tuzo za muziki za Mama’z zinazodhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel zinazoandaliwa na kituo cha luninga cha MTV Base ambazo zitafanyika ndani wiki tatu kutoka sasa jijini Lagos.

Wasanii hao pamoja na wasanii wengine kama Jozi kutoka Afrika kusini na Wande Coal kutoka nchini Nigeria wataungana na wasanii saba ambao tayari walikwisha thibitishwa kutoa burudani siku hiyo ya utoaji wa tuzo hizo.

Baadhi ya wasanii hao saba ni DJ Arafat (Ivory Coast), Daddy Owen (Kenya), and Fally Ipupa (DRC), ambaye pia alikuwepo jijini Lagos mwaka 2009.
Akizungumza jijini Nairobi baada ya kuthibitishwa kwa wasanii wa P unit, mkuu wa kitengo cha habari cha kampuni ya simu Airtel nchini Kenya Bw. Dick Omondi alisema, ‘Kuchaguliwa kwa wasanii hao watatu wanaounda kundi hilo la P Unit ni ishara ya kufanya vizuri kwa muziki wa Kenya barani Afrika.’

‘Sisi hapa Airtel tumepata faraja kwa wasanii wa Kenya kuchaguliwa kutumbuiza katika sherehe kubwa za kimataifa za muziki barani hivyo kuwa ishara kwetu kuwa muziki wetu unafanya vizuri”.

Michael Ross anawania tuzo ya msanii bora wa kimataifa katika tuzo hizo za Mama wakati kundi la muziki la P Unit lipo katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya kundi bora la muziki barani Afrika.

Kwa Rick Ross ambaye ana umri wa miaka 34, hii itakuwa mara yake ya kwanza kuja katika bara zuri la Africa na ii imetokea wakati muafaka ameachia albamu yake mpya inayoitwa “Teflon Don”.

Msanii huyo ambaye anajulikana kwa umbo lake kubwa pamoja na chata ya ndevu nyingi kidevuni na mashavuni ambaye anajulikana zaidi kwa nyimbo yake “Hustling” ambayo ilitoka mwaka 2006.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents