Burudani

Ride Along 2 yaongoza kwenye box office, yaitoa Star Wars: The Force Awakens kileleni

Filamu ya Star Wars: The Force Awakens wiki hii imeondolewa na filamu ya komedi, Ride Along 2 kwenye nafasi ya kwanza katika box office.

Filamu hiyo iliyochezwa na Kevin Hart na Ice Cube imeingiza dola milioni 34 Marekani na Canada tu hadi Jumapili. Ilianza kuoneshwa Ijumaa ya Jan 15. Hadi Jumatatu filamu hiyo inakadiriwa kuingiza dola milioni 45.

Filamu ya kwanza ya ‘Ride Along’ ilifanya vizuri pia kwa kuingiza dola milioni 48.6 Marekani katika uzinduzi wake. Hadi sasa imeingiza zaidi dola milioni 150.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents