Burudani

Tunda Man kuja na filamu fupi ya Mama Kijacho

Pamoja na video ya wimbo wake ‘Mama Kijacho’, Tundaman amesema ataachia filamu fupi yenye jina hilo.

Tundaman

Muimbaji huyo amesema filamu hiyo itakayokuwa ikielezea kisa cha Mama Kijacho itatoka baada ya video ya wimbo huo.

“Video tayari ila sasa hivi tupo kwenye mpango wa kushoot short film ya Mama Kijacho,” Tunda aliambia E-News ya East Africa Television Jumapili hii.

“Ndani ya filamu utawaona akina Riyama, mimi mwenyewe pamoja na wahusika wengine wengi. Nilishawahi kufanya filamu mara moja kwenye movie ya mtu ilikuwa hainihusu sana lakini hii inanihusu mimi kama mimi. Kwahiyo watu wasubirie kazi nzuri,” alisema.

Tunda amesema ameamua kumtumia Riyama na waigizaji wengine ili kuvutia na kuleta maana halisi ya wimbo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents