Burudani

Rihanna ‘am-unfollow’ Jennifer Lopez Instagram kufuatia tetesi za kutoka na Drake

Inaonekana kuwa Rihanna hajapendezwa na tetesi za ex wake Drake kuwa na uhusiano na Jennifer Lopez.

Watumiaji vinara wa mtandao wa Instagram, wamebaini kuwa Rihanna amem-unfollow J.Lo mwishoni mwa wiki na kupelekea watu kuamini kuwa Riri hajapendezwa na mrembo mwenzake huyo kutoka na ex wake, kama tetesi zinavyodai.

Drake mwenye miaka 30, na J.Lo, 47, walizalisha fununu za kupeana raha za dunia mapema mwezi huu baada ya Drizzy kuhudhuria show mbili za mrembo huyo jijini Las Vegas.

Jennifer na Rihanna, 28, ni marafiki wa muda mrefu licha ya kuwa na tofauti kubwa kiumri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents