Technology

RIPOTI: Huawei waigaragaza Apple kwenye mauzo ya simu janja ‘Smartphone’ duniani, Samsung waponea chupu chupu

Kampuni ya vifaa vya kielekroniki ya Huawei ya nchini China imeichakaza kampuni ya Apple kwenye mauzo ya simu janja ‘Smartphone’ duniani kote.

Image result for huawei hq

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Tafiti la Canalys and IHS Markit limeeleza kuwa Huawei wameuza simu milioni 54.2 kwa robo ya tatu ya mwaka 2018 ambapo ni ongezeko la 41% ukilinganisha na mwaka jana kwa kipindi kama hiki huku Apple wakiuza simu milioni 41.3 ambapo ni ongezeko la 1%.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa Samsung imeendelea kubaki kileleni kwa kuuza simu milioni 73.9 sawa na 20% ya soko lote duniani. Huawei wakiuza simu milioni 54.2 ikiwa ni sawa na 15% ya soko lote na Apple wakiuza simu milioni 41.3 ambapo ni sawa na 12% ya soko lote duniani.

Licha ya Samsung kukimbiza kwa mauzo ya simu janja duniani kwa robo tatu ya mwaka 2018, ripoti hiyo pia imeonesha kuwa kampuni hiyo imeshuka kimauzo kwa asilimia 10 kwenye soko la dunia ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka jana.

Makamu wa Rais wa Shirika la utafiti la IDC la nchini Singapore, Ryan Reith amesema kuwa Huawei matoleo mapya ya Huawei P20 Pro na yale ya Honor yamepokelewa vizuri duniani na ndiyo maana mauzo yameongezeka maradufu.

Ukuaji wa kampuni ya Huawei ni wa kasi sana hasa kwenye mauzo, ni ngumu kwa kampuni kama Huawei ambayo haina jina kubwa kupokelewa vizuri na bidhaa zake kununuliwa kwa kiasi hicho kwani ni ishara mwaka huu huenda tukaona mapinduzi kwenye mauzo ya bidhaa za kielekroniki,“amesema Ryan kwenye ripoti hiyo.

Kampuni ya Apple ilikuwa ikiongoza rekodi ya mauzo ya simu janja kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka kwa miaka mitatu mfululizo na ndio kampuni pekee  yenye thamani ya dola Trilioni $1 duniani.

Huawei wameizidi Apple kwenye mauzo ya Smartphone katika kipindi ambacho Kampuni hiyo ya China haijaanza kuuza bidhaa zake nchini Marekani.

 

Related Articles

6 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents