HabariMichezo

Robertinho kumpa jukumu maalum Sadio Kanoute

Licha ya kukiri utakuwa mchezo mgumu wa Derby ya Mzizima dhidi ya Azam FC leo, Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anawaamini wachezaji wake watawapa furaha ya ushindi.

Robertinho amesema wamepata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi zilizopita na wanajua umuhimu wake na amewasisitiza wachezaji mazoezini kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi wanazo tengeneza na kuzuia pamoja wanapo shambuliwa.

“Tuna matokeo mazuri kwenye ligi, tunatakiwa kuongeza kupata matokeo bora, tumetoka kupoteza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa hatutaki kupoteza tena kwakuwa itashusha morali yetu.

“Itakuwa mechi ngumu sababu ni Derby, Azam ni timu nzuri na tunaiheshimu lakini nawaamini wachezaji wangu watafanya vizuri,” amesema Robertinho.

Akizungumzia uwepo wa kiungo mkabaji, Sadio Kanoute ambaye alikosekana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Robertinho amesema:

“Nimefurahi kwa Kanoute kurejea kwenye mchezo dhidi ya Azam kwakuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza, uwepo wake unatupa machaguo mengi ya upangaji wa kikosi.”

“Pia Jonas Mkude ambaye alikuwa majeruhi nilimpa dakika 45 za mwisho kwenye mchezo uliopita na amefanya vizuri nimefurahi, anakuja kuongeza kitu kikosi,” amesema Robertinho.

Credit by @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents