Roma aelezea changamoto alizozipata katika zoezi la kuuza wimbo wake ‘2030’

Roma20301

Kama unakumbuka ROMA aliamua kuchukua uamuzi wa kuuza wimbo wake 2030 kwa kutumia M-Pesa kabla ya kuusambaza bure kwenye internet. Kupitia Facebook Roma amefunguka kuhusiana na changamoto alizokumbana nazo kwenye uuzaji wa ngoma hiyo:

Habari mabibi na mabwana!! poleni na mihangaiko ya siku!! naam

Ijumaa iliyopita nilitoa kibao changu maridhawa kipya kabisa kinaitwa 2030, na nilikiachia kwa radio stations zote nchini kadri ya uwezo wangu/wetu, though kutokana na mawasiliano ni ngumu kufikia radio zote kwa wakati, ila nyingi ziliupata!!!

Lakini niliweka utaratibu fulani kwa watakaohitaji kuupata huo wimbo 2030 mbali na radio basi wataupata kwa kussuport kuununua on line kwa tsh 3000/=!!nilishatangaza sana mnafahamu!!ilikuwa ni trial ya kuona nani ana love ya kussuport na nani hana kupitia njia zilizowekwa na sio njia nyingine.

Zoezi limeenda kwa challenge nyingi sana asante wote waliossuport katika hili, pia asante kwa wale walioliharibu zoezi hili maana imenifanya nimtambue hu z real na hu z fake!!!
Imeniuma kuona wapo wasanii wanafanya biashara kama hii wanauza mix tapes, album,tisherts zikiwa zote ni movements za kuleta changes ktk mziki wetu, then hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga hii movement yangu halafu bila sababu yani dah SHALL WE MAKE IT?????

Nway lilikuwa ni zoezi lililopangwa kufanyika kwa week moja 1 tu ili kuona na kufanya tathmini kuwa yanawezekana haya?najua wengi wanasubiri feed back ya mauzo haya haikuwa nzuri sana kwa wingi wa nyomi nililokuwa nalo, lakini pia haikuwa mbaya maana ni mageni haya..kwa siku 7 za mauzo ilikuwa kila siku wananunua watu wasiopungua 50!! so unaweza ona hapo kuwa yanawezekana haya tukiyawekea mkazo…ILA SIAMINI KAMA KILA MSANII ANAWEZA FANYA, INATEGEMEA NA NGUVU YA MSANII HUSIKA NA KIBAO ALICHOKITOA..(IFIKIE KIPINDI TUONGEE UKWELI TUU!!)

Wengi wameanza kufanya biashara kupitia nyimbo hii na inawanufaisha wao, wengi wamerecord radio wimbo huu kitu kilichopelekea kukosa quality na bado wanauzia wengine so wanapewa kitu kisicho na quality, pia wengi wanakwazika na mengi yaliyoongelewa ndani ya wimbo huu na wanakosa majibu maana wanakosa fursa ya kuusikia mara kwa mara kwasababu hawajaunga mkono hii movement!! au pengine imekuwa ni njia ngumu kwao kuupata.

Basi kwa wale waliossuport kwa kuinunua nawashukuru sana na mungu awaongezee mlipopungukiwa, najua litatokea hili la kujiona wanyonge kuwa ROMA amechukua fedha zetu na kisha ameachia bure, mi naamini ukiwa muelewa na ukiona nilichokisema hapo juu hautakwazika as long umeonyesha lav yako kwa msanii unayemfeel, samahani sana kama nitakuwa nimekukosea,nimefanya hivi kama kuanzisha hiki kitu na naamini wengine watafatia na kukiboresha zaidi!!LAZIMA APOTEE MMOJA ILI KUMI WAISHI VEMA NDIPO YATAPATIKANA MAENDELEO!! AM SO SORRY!!!

So leo wiki imetimia na wimbo umetoka rasmi na hauuzwi tena kama ilivyotangazwa awali.Na version iliyopita kuchezwa radio ni version ya ROMA ile beat yake iliyochangamka ambayo ni version ya 1 ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kutambulishwa ijumaa pale Clouds fm radio. Kwa maswali zaidi tutameet kwenye mainterviewz huko maradioni na tutawekana sawa!! Samahanini kwa wote niliowakwaza, asanteni kwa wote mliossuport!!

ROMA 2030 INAPATIKANA FREE SASA!!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents