Burudani

Roma atoa sababu za kwanini hutoa wimbo mmoja kwa mwaka

Rapper Ibrahim Musa aka ‘Roma Mkatoliki’ amesema kile kinachoonekanan kama ukimya wake kinatokana na desturi aliyojiwekea tangu aanze muziki wa kutoa wimbo mmoja kwa mwaka.

Roma...

Akizungumza na Bongo5 leo, Roma amesema ukiona yupo kimya katika muziki ujue anafanya shughuli za kiujasiriamali ambazo ni tofauti na muziki.

“Mwaka jana hakukuwa na kimya chochote kwa mtu anayemjua Roma kwa miaka yote,” amesema Roma. Roma kwa mwaka anatoaga wimbo moja. Kwahiyo mtu yoyote ambaye ana ‘judge’ kwanini Roma alikuwa kimya, ujue huyo kamjua Roma juzi.2007 ilitoka nyimbo ya kwanza, 2008 nyimbo ya pili, na nyimbo sita, kwahiyo kila mwaka natoaga nyimbo moja,sijawahi kutoa nyimbo mbili kwa mwaka. Kwa mwaka jana ni 2030. Nilikuwa kimya kwasababu ndio nyimbo iliyokuwa inachezwa.Na mwaka huu nitatoa nyimbo moja nanitakuwa kimya mpaka mwakani ndio kawaida ya Roma.”

“Nimeandaa nyimbo kama sita ndani ya ‘Tongwe records’ sema ni kuchagua nitoe nyimbo gani kwa mwaka huu. Sema nilikuwa kimya kidogo kutokana na majukumu ya maisha.Kama kawaida ya Roma ni nyimbo moja kwa mwaka, hata wimbo wangu 2030 ulitoka 28/12/2012. Lakini wimbo huu ni wa mwaka 2013 ndio maana ulipata air time nzuri 2013,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Roma amesema mwaka huu anatarajia kurudi shule baada ya kuhitimu na kushindwa kuendelea kutokana na muziki.

“Mimi ni mjasiriamali pia najarajia kurudi shule hivi karibuni,kwasababu nilihitimu nikashindwa kuendelea,ila mwaka huu nadhani suala la kurudi shule ni miongoni mwa mikakati yangu kwa mwaka huu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents