Burudani

Justin Bieber aharibu tena, akamatwa akiendesha gari akiwa amelewa

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Justin Bieber amekamatwa kwa kuendesha akiwa amelewa. Polisi wameuambia mtandao huo kuwa muimbaji huyo wa Canada alikamatwa Miami Beach kwa kosa la kuendesha akiwa amekunywa pombe (DUI) na kuendesha gari kwa kasi katika kile kilichodaiwa kuwa alikuwa akikimbizana na gari jingine.

Bieber Justin

Kukamatwa huko kumetokea asubuhi ya leo. Mtandao huo umesema kwa sasa Bieber anashikiliwa na polisi huku akitarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi. Inadaiwa kuwa Bieber alifanyiwa vipimo vya kutambua kama alikuwa amelewa na kushindwa.

Umesema kinachofuata ni kwenda jela ambako mambo ya dhamana yatafuata. Justin alikuwa anatoka club akiendesha gari aina ya Lamborghini lenye rangi ya njano. Vyanzo vimesema mtu aliyekuwa akikimbizana na Justin naye amekamatwa na alikuwa akiendesha Lambo ya rangi nyekundu.

Justin alikuwa amebeba msichana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents