Burudani

Roma auelezea wimbo wake mpya ‘Viva ROMA Viva’ utakaotoka 9/9

Roma anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Viva Roma Viva’ wiki ijayo sept 9.

Roma Viva

‘Viva Roma Viva’ ambayo tafsiri yake ni “LIVE LONG ROMA” ni single yake ya kwanza kutoka kwa mwaka huu.

Roma amepiga story na Bongo 5 na kuuelezea maana ya wimbo huo;

“Tafsiri yake ni “Live Long Roma”, Nikiwa na maana kuwa Jamii\Mashabiki\Uma unaonisikiliza umekuwa na Imani kubwa na Mimi pamoja na muziki wangu!kutokana na kile ninachokiwakilisha ktk Jukwaa LA HIPHOP! Imani hiyo inapelekea kufikia hatua ya Wananchi hadi Viongozi kunishawishi na kunishauri niingie kwenye jukwaa LA Siasa na nishike nafasi za uongozi!!Hiyo ni Imani waliyonayo kwangu kutokana na kile ninachokipigania kila Siku ktk tungo zangu! Nimekuwa nikiimba vitu ambavyo vinakuja kutokea baadae! Ingawaje mwanzo wakati vinatoka kuna wengine walidhihaki na kusema hizo ngonjera/mropokaji huyo!lakini baadae Yakima kutokea wanajirudi na kutoa credits kwangu na kukiri kuwa nafanya LIVING SONGS so hao hao mashabiki wanahitaji niendelee kuwepo hivyo wananiambia VIVA ROMA VIVA= LIVE LONG ROMA!!!!” alisema Roma.

Aliendelea;

“So ndani ya ngoma nimeongea mambo mengi sana!! Yanayofungua fikra za watu na kujua kuwa wapo bado ktk taifa la nmna gani na kipi cha kuchukulia hatua hasa ktk current situation!!!! Nimeongelea pia amani ya nchi na jinsi ya kuilinda/nimeongelea pia rais anayekuja na bunge litakalokuja no kipi wanapaswa wakifnye kwa wananchi wao ambacho hakijafanyka na Ndicho wananchi wanataka!! So haijaongelea matatizo tu!imeongelea na solution zake! Na ni wimbo ambao haujaegemea upande wowote ule wa chama wala Dini!”

Kuhusu ahadi aliyoitoa mwaka juzi ya kutoa single tatu kwa mwaka, Roma amesema mpango huo uko pale pale licha ya kuwa tuko mwezi Septemba na ndio anaachia wimbo wa kwanza.

“Kuhusu kutoa ngoma Tatu yeah sure zinatoka Tatu!! Na hadi sasa tumeshashoot ngoma ingine tofauti na hiyo Viva na imemalizika!! Na inatoka sambamba na hii VIVAROMAVIVA!!so naachia ngoma mbili kwa kufatana! Moja inakuwa video lakini nyingine ni kwa njia ya audio! Ngoma zimefanyika Home studio palepale Tongwe Records chini ya producer J Ryder!!!!”

Roma ambaye wimbo wa mwisho kuachia ulikuwa ‘Mwanakondoo’ ambayo ulitoka mwishoni mwa December 2014, amesema December ataachia single nyingine katika siku yake ya kuzaliwa.

“So zikitoka hizi mbili! Then December lazima niachie nyingine coz birthday yangu ni December 12 so kila Mwaka lazima niwabless na ngoma siku hiyo”.

Tunasubiri kuisikia ‘Viva ROMA ViVa’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents