HabariMichezo

Ronaldo akataa ukubwa ndani ya Al Nassr

Rais wa Klabu ya Al Nassr, Musalli Al Muammar amesema kuwa staa wa timu hiyo Cristiano Ronaldo ameomba atendewe sawa na wachezaji wenzake ndani ya kikosi, asipendelewe.

“Wakati wa makubaliano, Ronaldo aliomba atendewe sawa na wachezaji wengine kikosini, kwenye upande wa zawadi za motisha na kanuni za timu.”- Musalli Al Muammar

Rais huyo wa Al Nassr ameongeza kuwa mshahara wake ni wa juu zaidi, huku akishindwa kutaja kiasi halisi cha fedha na kuongeza makubaliano yao yanamanufaa ya faida za kibiashara pia.

“Makubaliano na Ronaldo hayaishii kwenye mpira pekee, atasaidia pia kwenye Al Nassr Club Academy mpango ambao tumepanga pamoja na kuiwakilisha historia ya klabu.”

Credit by @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents