Ruge Mutahaba: Beef ya Antivirus ilinifanya nikue


Jumamosi ya August 18 kwenye kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kupitia kituo cha radio cha Magic FM cha jijini Dar es Salaam, Ruge Mutahaba wa Clouds FM alifunguka kuhusu masuala mengi ya ndani kuhusu maisha yake, Clouds FM ilivyoanza, THT na namna beef yake na wasanii wa mixtape ya Antivirus iliyoongozwa na Sugu ambaye kwa sasa ni mbunge ilivyombadilisha. Hivi ndivyo alivyosema.
“Mimi nafikiri ilinifanya nikue, nikue kama nafsi, nafsi yangu ilikua, ilikomaa. Ilikomaa katika maana ya kuelewa kwamba…. ukaelewa ofcourse wanafiki ni nani, kuna watu wanashangilia panapotokea mikwaruzano au kutolewana kwa watu.Lakini kikubwa pia ambacho nilikiona ni kwamba kuna watu wanasubiri saa zote, wakisali mtu aanguke tu hata pasipokuwa na sababu ya kuanguka.

Kwasababu mara nyingi wanasema kwamba ukweli huwa unafungua vitu vingi sana na mara nyingi siri ya ukweli huwa ni muda, na mara nyingi ukikaa na wewe ukiwa mvumilivu na ukaamini kabisa kwamba there is nothing wrong with what I am doing, there is nothing.
Mimi natungiwa albam lakini nafikiria three quarters ya hawa watu mimi siwajui, hata sijawahi kufanya nao kazi hata siku moja, wengine hata kuwaona sijawahi kuwaona lakini wanakaa wanatunga nyimbo, mimi nawahusu vipi?
I like hiphop music , napenda kwa kusikiliza, lakini sijui, siwezi kusema hata siku moja kwamba ntaanzisha chuo au kituo cha kusaidia watu kwasababu sijui chochote kuhusu hip hop ntawaambia nini?
Kwahiyo sasa nikiambiwa sijui hip hop nawakandamiza, naanzaje kumkandamiza mtu! Wakati mimi sijui chochote kuhusu hip hop? Kwahiyo nasema kwamba anyway kuna watu wanafuata mkumbo bahati mbaya sana na ni vijana wengi bila kujua wanasema nini, na kuna wengine wanasahau kwamba ushindani ni mzuri lakini it’s supposed to be progressive kwa yoyote anayeshindana, the cake is always too big you can never think kwamba kwa kumbania huyu riziki yake… it wil never be like that.

I thank the Lord kwasababu nadhani ilinipa ujasiri sana, ilinikuza, yaani ilifika mahali ambako unakutana na watu wanakuogopa wewe kwasababu wanakufikiria Mungu wangu wanakutazamaje jana tu imetoka albam nyingine. Lakini mimi I was fine, I was happy and I got my strength from THT, from music. I think that was the time I got drown into music sana, sana, sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents