Habari

Rumors: Ndoa yanukia kati ya D’Banj na muigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji

Habari zilizoenea jijini Lagos nchini Nigeria zinadai kuwa wapenzi wa muda mrefu ambao waliwahi kuachana, mwimbaji wa kimataifa D’Banj pamoja na muigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji wamerudiana baada ya kuachana mwaka juzi.

Genevieve-Nnaji-DBanj
D’Banj na Genevieve

Habari za wapenzi hao kurudisha uhusiano wao zimesambaa katika siku kadhaa zilizopita na kuripotiwa na mitandao mbalimbali ya Naija.

Kwa mujibu wa habari zilizoenea kwenye mitandao, muigizaji huyo mrembo Genevieve alimwaga D’Banj mwaka 2011 kwa kile alichodai kuwa sababu ambazo haziwezi kutatulika baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka miwili, lakini hatimaye sasa wamerudiana.

Mtandao wa 360 Nobs umedai kuwa Genevieve amehamishia makazi yake kwenye nyumba ya hit maker wa ‘Oliver Twist’ D’Banj iliyoko Lekki, katika jiji la Lagos na kuwa wako serious zaidi na wana mpango wa kufunga ndoa hivi karibuni.

Hata hivyo si D’Banj wala Genny ambaye amezungumza chochote juu ya ndoa yao mpaka sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents