Habari

Sakata la sukari wafanyabiashara 84 wakamatwa, kufikishwa mahakamani

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa wafanyabiashara wa sukari 84 wamekamatwa na hivi karibuni watafikishwa mahakamani kutokana na kufanya ujanja ujanja katika suala la uuzaji wa sukari hapa nchini.

Bashe amebainisha hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari ambapo amesema oparesheni ya kuwakamata wafanyabiashara itaendelea mpaka pale bei itakaporudi kuwa kawaida.

Amesema wafanyabiashara wanamachaguo mawili moja waache kuuza sukari serikali itatafuta njia nyingine na wenye viwanda nao wanamachagua mawili wafuate utaratibu wa serikali na kama hawawezi waache hio kazi.

“Pia tumewapelekea walaka wa kubadilisha mfumo wa usambazaji, hiwezekani mfano Kagera Sugar anamsambazaji mmoja yupo Mwanza anahudumia mikoa 11, serikali haiwezi kuruhusu hili,” amesema Bashe na kuongeza

“Tuna changamoto kubwa ya wafanyabishara hasa wa retail kufanya uhuni hivyo mpaka sasa tupo katika hatua za mwisho kuwapeleka mahakamani, nini kinatokea sukari inaingia anauziwa kati ya 2500 hadi 2800 na importer, akinunua yeye anakwenda kuuza 4000 hadi 4500 wakati tayari sisi tumeshatoa bei elekezi

Amesema tatizo la bei sasa hivi ni la mpito, wanaamini mpaka kufika katikati ya mwezi Marchi watakuwa wameingiza nchini tani 60,000 za sukari, hivyo hadi kufikia mfungo wa mwezi wa Ramadhani hali itakuwa nzuri.

Waziri Bashe amesema wataendelea kuigiza sukari mpaka pale watakapoona stability ipo hivyo viwanda vinapoleta sukari mpaka kwa wauzaji wa jumla na kwamba kila atakayepewa sukari inayoagizwa kutoka nchp majina yake yatapelekwa kwa Wakuu wa Mkoa.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents