Burudani

Sarkodie wa Ghana achukua tuzo ya Headies Awards 2014 ambayo Diamond alikuwa akishindania

Jumapili Dec.14 nchini Nigeria zimetolewa tuzo za Headies Awards 2014 ambazo msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz alikuwa akishindania, lakini safari hii haikuwa bahati yetu kwasababu hakufanikiwa kushinda.

sarkodie

Sarkodie wa Ghana ndiye aliyeshinda kipengele cha BEST AFRICAN ARTISTE ambacho Diamond alikuwa akishindania. Wasanii wengine waliokuwa wakiwania kipengele hicho ni Mafikizolo (South Africa) pamoja na R2Bees (Ghana).

diamond2

Hicho ndio kilikuwa kipengele cha kilichoshindaniwa na wasanii wa nje ya Nigeria kwenye tuzo hizo zilizotolewa Jumapili Dec.14 siku moja ambayo na Miss World ilifanyika nchini Uingereza.

Katika tuzo hizo Davido alishinda tuzo mbili, ya msanii bora wa mwaka pamoja na wimbo wake ‘Aye’ ulishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka.

Wizkid alikuwa akishindania kipengele cha msanii bora wa mwaka, tuzo ambayo alishinda Davido.

Source: Pulse Nigeria

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents