Siasa

Sasa ruksa kumtembelea Bobi Wine na kuonana naye baada ya ulinzi mkali (+ Video)

Hatimaye jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine kumtembelea nyumbani kwake Magere anakozuiwa na vikosi hivyo kwa zaidi ya juma moja.

Hii ni baada ya mahakama kuu jana kutoa maamuzi ya ombi la Kyagulanyi na mkewe la kuondolewa kwa vikosi vya jeshi na polisi nyumbani kwake.

Kulingana na mwandishi wa BBC Issaac Mumena, mawakili hao waliruhusiwa kumuona baada ya kukaguliwa kwenye kizuizi cha jeshi kilichowekwa karibu na nyumbani kwake.

Kwa mjibu wa Asumani Basalirwa aliyezungumuza na BBC kwa njia ya simu, iliwachukua muda wa saa kadha kuwashawishi wakuu wa jeshi la UPDF na polisi kuweza kumuona mteja wao, lakini baadhi ya watu waliokwenda nao walibaki kwenye kizuizi cha jeshi akiwemo aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais Jenerali Henry Tumukunde.

Mwanasheria Basalirwa ameeleza kuwa wamemkuta Bobi Wine akiwa na upungufu wa chakula kutokana na kumzuia kutotoka nje na pia kuwazuia watu kuingia nyumbani kwake ambao wangemletea chakula lakini hali yake kiafya sio mbaya.

‘’Afya yake ni nzuri, hakuna kitu chochote lakini yeye anataka kitu kimoja tu nacho ni haki yake, anataka apewe uhuru kutoka kwake nyumbani kwenda kufanya kazi yake arudi’’, amesema Asumani Basalirwa.

Bobi Wine

Masuala muhimu yaliyowapeleka wanasheria hao kwa kiongozi wa chama cha NUP ni pamoja na kushauriana naye jinsi ya kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 14 mwezi huu wa Januari, yaliyompatia Rais Museveni ushindi wa kuongoza muhula wa sita.

Lakini je vikosi vya usalama vimewafahamisha kwanini wamemzuia Robert Kyagulanyi

Mwanasheria Asumani Basalirwa amesema,’’ walisema wao wako na intelijensia yao inayowaarifu kuwa Bobi Wine anafanya maandilizi ya kufanya makosa, ana mipango ya kufanya vurugu na kuwaambia raia waandamane barabarani.

Hii sio mara ya kwanza kwa jeshi la UPDF na polisi kuwazuia viongozi wa upinzani nyumbani kwao baada ya uchaguzi, Dkt. Kiiza Besigye baada ya uchaguzi wa mwaka 2016 alizuiwa nyumbani kwake Kasangati kwa zaidi ya miezi 3 hadi rais Museveni akaapishwa.

Hii itategemea uamuzi wa mahakama kuu wiki ijayo siku ya Jumatatu tarehe 25 baada ya Bwana Kyagulanyi na mkewe Babra Itungo kuomba mahakama kuwaondoa wanajeshi na polisi nyumbani kwake na kupewa uhuru wao wa kikatiba.

Bofya hapa kutazama zaidi.

https://www.instagram.com/tv/CKVzt_ehgRl/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents