Siasa

Serikali ya Kenya yakiri kukumbwa na ukata wa pesa

Serikali ya Kenya imekiri kwamba inakabiliwa na uhaba wa pesa ambao umechelewesha malipo ya mishahara ya maelfu ya wafanyikazi wa umma.

Inasema ilibidi kufanya maamuzi magumu iwapo italipa mishahara au kulipa mamilioni ya dola katika deni la nje, linalodaiwa mwezi huu.

Hazina ya kitaifa pia imeshindwa kutuma pesa kwa serikali za kaunti – vitengo vilivyogatuliwa ambavyo vinasimamia huduma za umma kama vile afya na elimu.

Wafanyikazi katika wizara, mashirika na serikali za kaunti ndio wameathiriwa zaidi na ucheleweshaji wa mishahara ya Machi.

Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u alisema serikali inakabiliwa na matatizo ya kifedha yanayosababishwa na mapato adimu na na mzigo wa madeni.

Vyama viwili vinavyowakilisha wafanyikazi wa serikali ya kitaifa na kaunti vimetoa notisi za nia yao ya kususia kazi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amelaumu mzozo huo kwa serikali ya zamani ambayo anaituhumu kwa kukopa pesa nyingi ikiwa mamlakani na kuvamia hazina kabla ya kuondoka mamlakani mwaka jana.Lakini hakutoa ushahidi wowote wa madai hayo.

Mshauri wa rais wa masuala ya uchumi David Ndii alisema mishahara iliyocheleweshwa sio shida na akataja hali kama “Changamoto ya upatikanaji wa hela”.

Katika mahojiano ya runinga, Bw Ndii alisema kuwa serikali ilikuwa inatarajia $500m (£460m) kutoka kwa mkopo ulioidhinishwa na mishahara ya watumishi wa umma italipwa mwishoni mwa wiki ijayo.

Deni la umma la Kenya sasa linafikia 65% ya mapato.

Nchi hiyo inahitaji zaidi ya $420m kila mwezi kulipa mishahara na pensheni kwa watumishi wa umma.

Credit by @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents