Habari

Serikali yaondoa ukomo matumizi ya vitambulisho vya Nida

Serikali imetangaza kuondoa ukomo wa Vitambulisho vya Taifa (Nida) vilivyomalizika muda wake baada ya kufanya mabadiliko ya Kanuni za Usajili na Utambuzi wa Watu za mwaka 2014.

Waziri, Mambo ya Ndani ya Nchi. Eng. Hamad Masauni (MB) amesema hayo akizungumza leo tarehe 21 Februari, 2023 na Waandishi wa Habari juu ya Marekebisho ya Kanuni za Usajili na Utambuzi wa Watu za mwaka 2014 ambapo kwa sasa Vitambulisho vya Taifa kwa raia, Vitaendelea kutumika bila kujali Muda wa Ukomo wa matumizi uliopo kwenye vitambulisho hivyo isipokuwa kwa wageni wakaazi na Wakimbizi.

Mchakato wa Marekebisho ya Kanuni umekamilika na tayari kanuni hizo zimeanza kutumika baada ya kutangazwa rasmi kwa tangazo la serikali (GN) Na 96 la tarehe 17 Februari 2023.

Serikali imetoa rai kwa watoa huduma wote nchini wanaotumia utambulisho wa Taifa kutoa huduma kwa wananchi hususan Taasisi za fedha, Benki na Kampuni za simu kuendelea kuvitambua na kuvitumia Vitambulisho vya Taifa ambavyo vina tarehe ya muda wa ukomo wa matumizi.

Credit by @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents