Habari

Pass Trust yazindua kampeni ya Kijanisha Maisha

Taasisi binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo (PASS) leo imezindua kampeni ya KIJANISHA MAISHA kwa wadau wake wa ndani ili kuelewa na kufahamu dhana hiyo inayotokana na mpango kazi wa kuhimiza kijani shirikishi. Dhumuni kuu la uzinduzi huo ni kukuza mageuzi ya biashara ya kilimo katika sekta ya kilimo.

Uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust ambapo aliweka wazi jinsi KIJANISHA MAISHA itakavyochukua jukumu muhimu katika kuleta maendeleo ya sekta ya kilimo. KIJANISHA MAISHA ni kampeni mwamvuli yenye wito wa kuhamasisha wadau wote wa kilimo biashara kufuata kanuni za uzalishaji zinazofuata ukuaji wa kijani shirikishi ambazo ni pamoja na; Matumizi bora ya maliasili, ulinzi wa makazi unaojumuisha bioanuwai na mifumo ikolojia yake, uzalishaji kidogo wa hewa ya kaboni ili kupunguza kiwango cha kaboni, ushirikishwaji wa wanawake na vijana, usawa na haki ya kijamii, uvumbuzi na uundaji wa ajira ya kijani shirikishi.

, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo (PASS Trust), Yohane Kaduma,akiongea leo katika uzinduzi wa kampeni ya KIJANISHA MAISHA kwa wadau wake wa ndani ili kuelewa na kufahamu dhana hiyo inayotokana na mpango kazi wa kuhimiza kijani shirikishi. uzinduzi huu umefanyika leo Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya KIJANISHA MAISHA, Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Kaduma alisema: “Kilimo kinacho zingatia ukuaji wa kijani shirikishi kitasaidia wadau wa kilimo biashara kutoka sekta ya uvuvi, ufugaji, na misitu kupata mikopo kutoka taasisi za fedha kupitia mfumo wa udhamini wa mikopo wa PASS.  Ambapo wajasiliamali hao  wana nafasi ya kupata dhamana ya mikopo ya hadi 80%”.

Kaduma anaongeza kuwa “Katika dunia ya sasa mabadiliko ya hali ya hewa ni ajenda kuu ya kimataifa. Ambapo PASS Kama mawakala katika kufanya mabadiliko kupitia sekta ya kilimo tunahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wote muhimu wakiwemo watoa huduma za Kifedha, asasi za kiraia, mashirika ya mazingira,na wafadhili wa mashirika mengine wa ili kufikia lengo moja la mabadiliko ya kilimo biashara kwa kuzingatia ukuaji wa kijani shirikishi ambao utachochea ukuaji wa kilimo endelevu”

Akielezea namna wakulima walivyo katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia kampeni ya Kijanisha maisha.  Kaduma alisema: “Inawezekana baada ya miaka michache tukawa katika kiwango kizuri kiuchumi kwa sababu Kijanisha maisha itachochea kilimo endelevu ambacho kitakuwa na manufaa kwa  biashara ya kilimo nchini”.

Tangu kuanzishwa kwa Kijani shirikishi , mpaka Desemba 2022, jumla ya miradi ipatayo 66, 077 zilinufaika na dhamana kutoka PASS, zikiwafikia takribani wanufaika 3,427,960 na kutengeneza ajira zipatazo 2,712,048

PASS inapatikana nchi nzima kupitia ofisi zake za kanda zilizopo kama ifuatavyo, Kanda ya Ziwa, Mwanza; Kanda ya kati na mashariki, Morogoro; kanda ya kusini, Ruvuma; kanda ya kaskazini, Arusha; Kanda ya magharibi, Tabora; Kanda ya nyanda za juu kusini, Mbeya na makao makuu yake, Dar es salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents