HabariMichezo

Simba wajipongeza kwa sare vs Azam

Licha ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya Azam FC kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kupambana kutafuta alama tatu ingawa hatukufanikiwa.

Robertinho amesema wamecheza vizuri lakini bao la mapema kipindi cha kwanza liliwafanya kutoka kwenye mfumo uliowafanya kupoteza nafasi.

Mbrazil huyo amedai kuwa kipindi cha pili alibadili mfumo kwa kuwaingiza washambuliaji watatu wenye kasi ili kuwafungua Azam ambao mara nyingi walikuwa nyuma.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wangu, wamejitahidi kupambana kutafuta ushindi. Tulitamani kupata pointi zote tatu lakini lazima tukubali tulichojaaliwa na huu ndio mpira.

“Baada ya kuruhusu bao la mapema kipindi cha pili tulibadili mfumo na kutumia washambuliaji watatu ili kuongeza presha na kuwafanya Azam kufanya makosa.

“Tulimuingiza Jean Baleke, Habib Kyombo na Kibu Denis na kuwatoa Pape Sakho, Saido Ntibazonkiza na John Bocco ambao waliongeza kasi na tulibadili hali ya upepo na kupata bao la kusawazisha,” amesema Robertinho.

Robertinho amewapongeza mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ingawa hatujapata matokeo ya kufurahisha.

Credit by @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents