Habari

Shambulio la kigaidi laua sita London (+video)

Watu sita wameripotiwa kufariki dunia na wengine kadha kujeruhiwa katika tukio lililohusisha watu kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu katika eneo la Daraja la London nchini Uingereza.

Polisi na magari ya kubebea wagonjwa katika upande wa kusini wa Daraja la London
Polisi na magari ya kubebea wagonjwa katika upande wa kusini mwa Daraja la London

Polisi wa uchunguzi nchini Uingereza wamesema walipokea taarifa za watu kugongwa kwa gari katika daraja hilo huku watu 48 wakijeruhiwa vibaya na watu watatu waliokuwa wameshika visu katika soko la Borough.

Polisi Jijini London, wanasema kuwa matukio yote mawili yanachukuliwa kama matukio ya kigaidi yanayoendelea nchini Uingereza.

Kwa miezi mitatu mfululizo Uingereza imekuwa ikiandamwa na matukio ya mashambulio ya kigaidi hasa kwenye miji ya London na Manchester.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents