Burudani

Shetta: Nimeanza kupata maombi ya Interviews kwenye radio za Nigeria

Msanii wa Tanzania kupata nafasi ya wimbo wake kuchezwa hadi kuingia kwenye Top 10 ya radio tatu za Nigeria ni jambo kubwa, lakini kufikia hatua ya hadi kuombwa kufanyiwa mahojiano na radio hizo ni jambo kubwa zaidi ambalo tunaweza kulihesabu kama sehemu ya mafanikio kwa msanii wa bongo aliyeianza safari ya kujitangaza kimataifa.

shettaa

Wimbo wa Shettah aliomshirikisha Diamond Platnumz ‘Kerewa’ ulianza kuvuka mipaka baada ya kutoa video aliyoshoot Afrika Kusini na mmoja wa madirector wakubwa wa Africa aitwaye Godfather, na hatimaye ulifanikiwa kuingia kwenye Top 10 ya Naija 102.7 FM, City 105.1 FM na The Beat 99.9 FM zote za Nigeria.

Shettah ameiambia Bongo5 leo kuwa kwa sasa ameanza kupokea maombi ya Interviews kutoka Radio za Nigeria.

“Nimepata kama email mbili tatu kutoka kwa mmoja wa watangazaji wa Nigeria, kuna ile City Fm, walikuwa wanataka Interview wananiambia kuna demand kubwa ya fans wangu Nigeria wanataka kusikia nini naongea, nimewaambia wanitumie maswali kwaajili ya Interview”.

Shetta ameongeza kuwa kuna project mpya inakuja kutoka kwake lakini hayuko tayari kuizungumzia kwa sasa hadi atakapokamilisha mipango yote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents