HabariUncategorized

Shuhudia nyuki walivyoivamia Ndege hii nchini Afrika Kusini

Shuhudia nyuki walivyoivamia Ndege hii nchini Afrika Kusini

Nyuki waliyoingia kwenye injini ya ndege ya shirika la Mango wamesababisha kuchelewa kwa safari za ndege katika uwanja mkuu wa ndege mjini Durban,Afrika Kusini. Wataalamu wa nyuki waliitwa kuja kusaidia kuwaondoa nyuki hao karibu 20,000 kutoka kwa injini ya ndege hiyo.

Mmoja wa wataalamu hao amesema tukio hilo si la kawaida na kwamba huenda nyuki hao walikua wakipumzika kabla ya kuelekea mahali pengine. Ameongeza kuwa hawakua na mpango wa kuishi ndani ya injini iliyo na ”harufu kali”.

Nyuki hao walijaa ndani ya injini ya ndege ya shirika la Mango chini ya dakika 25, hali ambayo ilisababisha ndege zingine tatu kuchelewa kuondoka katika uwanja wa Kimataifa wa King Shaka. Msemaji wa shirika la ndege la Mango, Sergio dos Santos amesema ”Sijawahi kuona kisa kama hiki katika kipindi cha miaka minane niliyohudumu katika shirika la ndege”

Shirika hilo pia limeandika kuhusu tukio hilo katika mtandao wake wa Twitter:

Ilichukua muda kabla ya watalamu hao kuruhusiwa kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwa sababu walihitaji idhini kutoka kwa mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege nchini.

Melvyn Dawson, mmoja wa wataalamu wa nyuki alisema ilikua ”kazi rahisi” na kwamba walichohitaji ruhusa tu ya kufikia ndege hiyo.Akizungumza na shirika la habari la News24 Dawson, alisema, “Tumekumbana na visa kadha vya kuondoa nyuki waliovamia mahali fulani lakini sijawahi kuona kisa kama hiki”.

Ameongeza kuwa nyuki hao wamehifadhiwa nyumbani kwa ndugu yake ambaye pia ni mfugaji nyuki na kwamba watapelekwa mashambani hivi karibuni.

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents