Burudani

Sikuwahi kuondoka MJ Records – Joslin

Rapper Joslin amedai kuwa hajawahi kuondoka MJ Records wala kuwa na ugomvi na label hiyo.

Rapper huyo wa Wakali Kwanza, amemuambia mtangazaji wa kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Raheem Da Prince kuwa uzushi wa watu ndio uliofanya ionekanae kama amezinguana na MJ Records.

“Ni mambo ya kibiashara tu, kwamba kuna kipindi ilifika mimi nikaenda kufanya kazi kwa J Murder Tongwe Records, na nimefanya kazi nyingi tu pale, nimefanya album karibu mbili lakini unaweza ukasikia nyimbo mbili au tatu na Jose Mtambo ile,” alisema.

Kwa upande mwingine, Joslin alisema yeye na Mr Blue hakuwahi kuwa na bifu bali ilionekana kuwepo tu kwenye vyombo vya habari. Kwa sasa Jos anasema ili aweze kurejea tena vizuri kwenye game, anahitaji management ya maana na sio wababaishaji. Ametoa wito kwa wadau wenye uwezo waweze kuwekeza kwenye muziki wao.

Rapper huyo amedai kuwa yeye na kundi lake na Wakali Kwanza wamesharekodi nyimbo tisa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents