HabariMichezo

Simba imemsajili ‘Bale’

Tetesi zinasema Simba imefanikiwa kuidaka saini ya kinda kutoka Tanzania Prisons winga Edwin Balua ambaye amekuwa na msimu Bora sana akiwa na maafande hao wa prisons na kumpelekea kuitwa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Bwana mdogo tangu yupo mdogo jina lake la utani au jina lake maarufu anaitwa Bale alipewa jina Hilo ni kutokana kufanana sana kiuchezaji na mchezaji wa Zamani wa Tottenham Hotspur pamoja Real Madrid Galeth Bale wote wakiwa na speed wana ngumu wanauwezo wa kupiga mashuti kupiga mipira ya Faulo na wanatumia miguu ya kushoto ndiyo wakambatiza jina la bale .

Winga Huyo ameshawahi kupita katika klabu ya DTB ikiwa daraja la pili na kuipandisha daraja la kwanza na baadae kwenda ligi kuu Zanzibar akacheza kwa msimu mmoja na baadae kupata nafasi ya kujiunga na klabu ya wagosi wa kaya Coastal Union ya Tanga lakini hakupata sana nafasi sababu ya kupata majeraha na kocha kutompa nafasi msimu uliopita alijiunga na Prisons.

Nyota yake ikaanza kung’aa na klabu hiyo kutoka mbeya kabla ya kuanza msimu huu mpya alipata dili tatu mbili nchini Norway Moja bongo katika klabu ya Ihefu FC na katika dirisha dogo Simba wamevutiwa nae na kuamua kumsajili na menejementi yake kuamua kuachana na dili za ulaya na kuamua kukubali ofa nzuri ya klabu ya Simba.

NB:Simba Imemsajili Bale.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents