Michezo

Simba waanika mapato ya mechi ya watani wa Jadi, waipeleka Yanga kwa pilato ‘Tumechukua hatua’

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC hii leo siku ya Alhamisi wametoa jumla ya makusanyo ya fedha yaliyopatikana kwenye mchezo wao dhidi ya watani zao wa jadi Yanga SC.

Katika taarifa hiyo ambayo wameitoa kupitia akaunti yao ya kijamii ya Intsagram, Simba imesema kuwa jumla ya makusanyo yalikuwa ni Tsh 539, 120,000.

Kwa upande mwingine Wekundu hao wa Msimbazi wamesema kuwa wameguswa na kauli ambazo zimetolewa kabla ya mechi na viongo wa Yanga SC hata hivyo hawakuzieleza kauli hizo.

Simba SC wameongeza kuwa wanazikemea kauli hizo zisizo na tija na zenye lengo za kuaribu taswira na heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini.

Hata hivyo kupitia taarifa hiyo Simba imesema kuwa imechukua hatua ya kufikisha malalamiko yao dhidi ya kile walichokieleza ni kauli hizo mbele ya Bodi ya Ligi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents